Swalah kwenye msikiti ulio karibu na makaburi

Swali: Je, inasihi kuswali kwenye msikiti ulio karibu na makaburi na hayako ndani yake?

Jibu: Ikiwa makaburi yako nje ya msikiti na kati yake kuna uwazi pengo kama njia, barabara au utupu kati ya msikiti na makaburi haidhuru. Aswali kwenye msikiti huo kwa kuwa haina makaburi.

Ikiwa kaburi limeambatana na msikiti swalah haisihi katika msikiti huo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020