Swali: Mmetaja maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu swalah ya ´Ishaa:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokana na misikiti ya Allaah.”
Kisha kumepokelewa kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) ambaye amesema:
“Lau Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) angejua yale ambayo wanawake wamezua leo, basi angewazuia.”
Je, vipi tutaweza kuoanisha kati ya mawili hayo?
Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mwekaji Shari´ah kutoka kwa Allaah (Ta´ala) na ndiye mwenye kufikisha kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Yeye ndiye aliyesema:

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Anapokuomba mke wako ruhusa ya kwenda msikitini, basi usimzuie.”
Baadhi ya watoto wa ´Abdullaah bin ´Umar waliposema:
“Tunaapa kwa Allaah tutawazuia.”
Kwa sababu ya hali walizoona. Ndipo ´Abdullaah bin ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) akawakaripia vikali kwa sababu wamepingana na Sunnah kwa maoni yao mwenyewe.
Sunnah imethibitisha kuwa wanawake hawazuiliwi kwenda misikitini, lakini kwa masharti. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwanamke yeyote atakayejipaka ubani, basi asihudhurie nasi swalah ya ´Ishaa.”
Pia aliwahimiza juu ya sitara, Hijaab na kujisitiri. Kwa hiyo mwanamke hatakiwi kuzuiliwa ikiwa atatoka kwa adabu na kujisitiri kikamilifu. Lakini ikiwa mwanamke anasababisha fitina kwa kuonyesha mapambo, kujipamba kupita kiasi au kutoka na manukato yanayopenya kwa watu, basi atazuiwa, kama yalivyofahamisha maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mwanamke yeyote anayejipaka ubani, basi asihudhurie nasi swalah ya ´Ishaa.”
Hii inajulisha kuwa hatakiwi kutoka na manukato ya aina yoyote yanayofika kwa watu. Aidha ni lazima awe amejisitiri na siyo mtu wa tuhuma. Ikiwa anatumia kwenda msikitini kama kisingizio cha mambo yanayomdhuru mumewe au familia yake, basi anazuiwa.
Kwa kumalizia ni kwamba mwanamke hazuiliwi ikiwa ni mwenye tabia njema, mwenye kujisitiri, haendi kinyume na maamrisho ya Allaah na kutoka kwake kunamnufaisha bila kuleta madhara kwa watu. Hapo hakuna tatizo.
Kuhusu maneno yake ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa):

Jibu ni kwamba Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) anajua kila kitu. Isitoshe Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hafanyi jambo kwa matamanio yake. Allaah (Ta´ala) anajua yaliyotokea wakati wa ´Aaishah, yaliyopo leo na yatakayokuja baada ya karne nyingi. Pamoja na hayo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ametuwekea Shari´ah kuwa tusizuie wanawake. Kwa hiyo maneno ya ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) katika suala hili si yenye kutegemewa. Bali kinachotegemewa ni Sunnah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah anajua yaliyokuwa, yatakayokuwepo katika karne ya kumi na nne, kumi na tano, kumi na sita na baadaye. Shari´ah ni ya wote; ya Maswahaba, ya watu wa karne hizi na ya watakaokuja. Hivyo maneno ya ´Aaishah hapa ni jitihada yake na jitihada inaweza kupatia au kukosea.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1054/السنة-في-خروج-النساء-للمساجد
- Imechapishwa: 22/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1054/السنة-في-خروج-النساء-للمساجد
Imechapishwa: 22/01/2026
https://firqatunnajia.com/wanawake-kwenda-kuswali-misikitini-katika-zama-za-fitina/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket