Swali: Ni sababu gani iliyomfanya Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) achague du‘aa ya kufungulia swalah:
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ وتَبَارَكَ اسْمُكَ وَتَعَالى جَدُّكَ وَلا إِله غَيْرُكَ
“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, kutokamana na kasoro zote na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, ufalme Wako ni mkubwa na hapana mungu wa haki mwengine asiyekuwa Wewe.”[1]
ilhali Hadiyth hii ambayo cheni yake ya wapokezi imekatika, kama walivyosema wanazuoni wa Hadiyth? Isitoshe inajulikana kuwa Imaam Ahmad ameacha baadhi ya Hadiyth Swahiyh kuhusu jambo hili?
Jibu: Hadiyth hii imekatika katika njia ya ‘Umar (Radhiya Allaahu ´anh), lakini imepokelewa kwa njia nyingine ambazo hazijakatika. Imepokelewa pia kutoka kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), Abu Sa‘iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) na [Abu Hurayrah]. Du‘aa hii ni fupi sana na ni ibara safi ya kumtaja Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Kwa sababu hiyo waliipendelea wale waliopendeza du‘aa hii ya kufungulia swalah, kwa kuwa ni Dhikr tupu. Haini maombi, bali yote ni kumsifu Allaah (Ta´ala). Pia ni fupi na rahisi kuhifadhiwa na watu. Kwa sababu hizo Imaam Ahmad na wengineo waliipendelea bila kupinga du‘aa nyingine za kufungulia swalah. Hii ni du‘aa fupi na yenye uwazi na imepokelewa katika Hadiyth mbalimbali. Ndiyo maana kundi la wanachuoni walipendelea kuitumia kutokana na ufupi wake na kuwa kwake Dhikr safi ya kumsifu Allaah (Subhaanah).
Mtu akifungua swalah kwa du‘aa nyingine, kama mfano wa:
اللَّهُمَّ بَاعِدْ بَيْنِي وَبَيْنَ خَطَايَايَ كَمَا بَاعَدْتَ بَيْنَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ، اللَّهُمَّ نَقِّنِي مِنْ خَطَايَايَ كَمَا يُنَقَّى الثَّوْبُ الْأَبْيَضُ مِنَ الدَّنَسِ، اللَّهُمَّ اغْسِلْني مِنْ خَطَايَايَ، بِالثَّلْجِ وَالْماءِ وَالْبَرَدِ
“Ee Allaah! Niweke mbali mimi na makosa/dhambi zangu kama ulivyoweka mbali baina ya mashariki na magharibi. Ee Allaah! Nitakase na makosa/dhambi zangu kama Unavyoitakasa nguo nyeupe na uchafu. Ee Allaah! Nisafishe na makosa/dhambi zangu kwa theluji, kwa maji na kwa barafu.”[2]
للَّهُمَّ رَبَّ جِبْرِيلَ وَمِيكَالَ وَإِسْرَافِيلَ فَاطِرَ السَّمَواتِ والأَرْضِ عَالِمَ الْغَيْبِ والشَّهَادَةِ أَنْتَ تَحْكُمُ بَيْنَ عِبَادك فِيما كانُوا فِيهِ يَخْتَلِفُونَ اهْدِنِي لِمَا اخْتُلِفَ فِيهِ مِنَ الْحَقِّ بإِذْنِكَ إِنَّكَ تَهْدِي مَنْ تَشَاءُ إِلى صِرَاطٍ مُسْتَقِيم
“Ee Allaah! Mola wa Jibriyl, Mikaaiyl na Israafiyl! Muumba wa mbingu na ardhi! Wewe ambaye ni Mjuzi wa mambo yenye kujificha na yalio ya wazi! [Siku moja] utahukumu baina ya waja Wako katika mambo ambayo walikuwa wakitafautiana! Niongoze mimi katika haki katika yale waliotafautiana kwa idhini Yako, kwani hakika Wewe unamuongoza umtakaye katika njia ilionyoka.”[3]
Zote ni nzuri. Bora zaidi ni kwamba mtu abadilishe; mara atumie hii, mara nyingine atumie ile ili akusanye aina zote za du´aa za kufungulia swalah.
[1] Muslim (399).
[2] al-Bukhaariy (744) na Muslim (598).
[3] Muslim (770).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1073/سبب-اختيار-الامام-احمد-دعاء-الاستفتاح-سبحانك-اللهم-وبحمدك
- Imechapishwa: 22/01/2026

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1073/سبب-اختيار-الامام-احمد-دعاء-الاستفتاح-سبحانك-اللهم-وبحمدك
Imechapishwa: 22/01/2026
https://firqatunnajia.com/kwanini-wanazuoni-wakapendekeza-duaa-hii-ya-kufungulia-swalah/