Wanawake kujitia manukato mbele ya mwalimu wa kiume kipofu

Swali: Mwalimu ambaye ni kipofu katika moja ya shule za wasichana wakati mwingine wanafunzi hao wa kike au waalimu wa kike wanakuwa wenye kujitia manukato. Ni ipi hukumu ya hilo kwa sababu mwalimu huyo huhisi kwa pua harufu yao?

Jibu: Wanatakiwa kuacha kujitia manukato. Anatakiwa kuzungumza nao ikiwa wanachanganyikana na wanamme. Ni mamoja wakiwa waalimu hao wakike au wasiokuwa hao. Wanalazimika kuachana na jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21920/حكم-تعطر-النساء-عند-المدرس-الاعمى
  • Imechapishwa: 01/10/2022