Wanataka tujiunge na Jamaa´at-ut-Tabliygh na al-Ikhwaan

Swali: Sisi ni vijana tunaitwa katika wapendwa na al-Ikhwaan. Ni ipi nasaha yako?

Jibu:

وَاعْتَصِمُوا بِحَبْلِ اللَّـهِ جَمِيعًا وَلَا تَفَرَّقُوا

”Na shikamaneni kwa kamba ya Allaah nyote pamoja, wala msifarikiane.” (03:103)

Nchi hii kuna kundi limoja. Liko juu ya Tawhiyd na Dini ya sahihi. Imekuwa hivo kwa kizazi baada ya kizazi. Kwa nini tufungue njia ya makundi na madhehebu? Kwa nini tufarikiane?

Kwa nini watu hawa wanajitenga na sisi na wanajiita kwa jina maalum ikiwa kama kweli ni wema? Hatukubali mfarakano. Hatukubali majina mengi. Sisi ni kundi limoja:

هُوَ سَمَّاكُمُ الْمُسْلِمِينَ

“Yeye (Allaah) Ndiye Aliyekuiteni Waislamu.” (22:78)

Hatukubali mgawanyiko huu. Huu ndio msingi wa kuufarikanisha Ummah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/ls–14330126.MP3
  • Imechapishwa: 22/04/2015