Wanataka kuhamisha makaburi kwa ajili ya barabara

Swali: Kijijini mwetu kuna makaburi ya zamani na kuna barabara na hakuna barabara nyingine. Je, tuhamishe makaburi tunayotembea juu yake na pambizoni mwake kuyapeleka maeneo mengine?

Jibu: Makaburi hayo na wakazi wa makaburi hayo wamekutangulieni. Kwa hivyo wao ndio wanamiliki maeneo hayo ambayo wanakaa. Hivyo basi, haijuzu kuyahamisha na kutembea juu yake. Yaheshimuni na tafuteni njia nyingine kama mlivokuwa mnafanya hapo kabla. Yaacheni makaburi kama yalivyo.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-نقل-المقبرة-التي-يمر-بها-طريق-إلى-مكانٍ-آخر
  • Imechapishwa: 12/06/2022