Swali: Ni jambo lisilofichika kwenu kuenea kukubwa kwa filamu za video na kusambaa kwake kati ya waislamu katika masomo na majumba yao. Hapana shaka kwamba ni kitu kina taathira kubwa juu ya ´Aqiydah, maadili na tabia ya waislamu. Ni ipi hukumu ya kutazama filamu hizi? Ni ipi hukumu ya kuzinunua, kuziuza na kukodisha maduka yake? Wanazuoni na watu wengine wana jukumu gani juu yake?

Jibu: Ni jambo linahitaji upambanuzi. Ikiwa kunauzwa ndani yake kitu kinachodhuru maadili na kuidhuru dini basi ni haramu. Serikali imesambaza marufuku juu ya hili, baraza la Kibaar-ul-´Ulamaa wameandika juu yake na mamlaka husika imepiga marufuku ya kukataza aina zote za filamu mbaya. Ambaye anajua kitu kibaya basi ni lazima kwake kukikemea. Haijuzu kuiuza wala kuinunua. Ni lazima kwa waislamu kunasihiana na wamshtaki yule anayeuza filamu chafu na amkemee mpaka kuhakikike jambo la kushirikiana katika wema na kumcha Allaah na kuusiana kunako haki. Hii ni dini ya Allaah. Hivyo ni lazima kusaidiana.

Filamu ambazo zinaeneza maovu, zinaonyesha kuchanganyikana kwa wanawake na wanamme, mwanamme dhidi ya mkewe, mwanamme akimlawiti wanamme mwenzie na mengineyo katika aina ya maharibifu, ni maovu makubwa na haijuzu kuziuza, kutangamana nazo wala kuzichukua kopi. Bali ni lazima kuzikemea na kuzipasua. Ni lazima vilevile kumshtaki mwenye nazo na kubainisha hali yake ili ziondoke shari hizi na waislamu wasalimike kutokana na shari yake. Haijuzu kuziuza wala kuzinunua kwa hali yoyote. Tunamuomba Allaah aiwafikishe serikali kufanya kile kinachotakiwa kwa njia kamilifu zaidi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4309/حكم-الفيديوهات-التي-تهدم-العقيدة-والاخلاق
  • Imechapishwa: 16/06/2022