Swali 123: Ni yepi maoni yako juu ya ambaye anawajibisha Jihaad katika wakati wetu wa sasa? Endapo atatoka mmoja kwa ajili ya Jihaad anapata dhambi?

Jibu: Jihaad haiwi isipokuwa ikitimiza vidhibiti na masharti yake. Lakini midhali haikutimiza masharti na vidhibiti vyake, basi hapo hakuna Jihaad inayokubalika Kishari´ah. Kwa sababu itawapelekea zaidi madhara waislamu kuliko yale manufaa machache. Kwa hivyo kitendo hichi hakijuzu. Muda wa kuwa Jihaad haijatimiza masharti na vidhibiti vyake pamoja na kiongozi muislamu na uongozi wa Kiislamu basi hakuhakiki Jihaad. Ingawa makusudio ya mtu ni mema na anachotaka ni Jihaad na analipwa kwa nia yake. Lakini pamoja na hivyo yeye ni mwenye kukosea katika jambo hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa ´Ulamaa-ul-Kibaar fiy al-Irhaab wat-Tadmiyr, uk. 307
  • Imechapishwa: 02/11/2019