Wanaoshirikiana kichinjwa kimoja cha Udhhiyah kukata nywele zao

Swali: Masikini wameshirikiana katika kchinjwa cha Udhhiyah. Je, wote wanatakiwa kujizuia kukata nywele zao?

Jibu: Sijui msingi wa hilo. Isipokuwa ikiwa ni wakazi wa nyumba moja hapana vibaya.

Swali: Wanaishi katika nyumba moja, lakini sio ndugu.

Jibu: Hapana vibaya ikiwa ni wakazi wa nyumba moja. Wote wajizuie kukata nywele na kucha au msafara mmoja kama wanaoishi nyumba moja.

Swali: Je, ni sharti wawe wanatokana na familia moja?

Jibu: Hapo ni pale ambapo wanaishi katika nyumba moja hata kama sio wanandugu, kwa sababu wamekuwa ni watu wa nyumba moja. Hadiyth inasema:

“Kichinjwa kimoja kinamtosha mtu yeye na watu wa nyumbani kwake.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21838/حكم-اخذ-الشعر-للمشتركين-في-اضحية
  • Imechapishwa: 08/06/2024