Swali: Baadhi ya watu kwa masikitiko makubwa utawaona katika Ramadhaan wanachunga vipindi vya swalah vitano, swalah ya Tarawiyh, Tahajjud na kusoma Qur-aan. Ramadhaan inapomalizika wanaacha sehemu kubwa ya mambo hayo. Ni ipi hukumu? Je, matendo yao mema hayo yanakubaliwa katika Ramadhaan?

Jibu: Ni jambo zuri kujitahidi kwa matendo mema katika Ramadhaan. Ramadhaan ina sifa zake za kipekee na ni msimu mtukufu. Lakini kinachotakikana kwa muislamu ni yeye kujitahidi matendo mema katika umri wake wote, katika maisha yake yote na katika miezi yote. Umri wake ni fursa yenye thamani. Ni mwenye kwenda katika nyumba inayohitaji matendo. Hakika si venginevyo malipo huko Aakhirah yanatokana na matendo. Muislamu anatakikana atumie maisha yake ulimwenguni katika matendo mema. Ayafanye maalum masiku yenye ubora, misimu yenye kheri, kama vile Ramadhaan, kwa kujipinda zaidi.

Kuhusu watu hawa ambao wanazembea na kupuuza mambo ya faradhi na swalah na pindi inapofika Ramadhaan ndio wanajitahidi na kuhifadhi swalah na pindi Ramadhaan inapomalizika, basi wanaacha mambo ya faradhi na kuyapoteza, watu hawa haikubaliwi ijtihadi yao katika Ramadhaan. Baadhi ya Salaf waliambiwa:

“Kuna watu wanaojitahidi ndani ya Ramadhaan na inapomalizika wanaacha matendo.” Wakasema: “Ni watu waovu kabisa gani. Hawamjui Allaah isipokuwa katika Ramadhaan.”

Watu hawa hayakubaliwi kutoka kwao wakiacha mambo ya faradhi na swalah tano. Hata hivyo hapana neno endapo inahusiana na kuacha kitu katika mambo yaliyopendekezwa. Inatarajiwa kukubaliwa katika yale yaliyopita katika Ramadhaan.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (02/385-386)
  • Imechapishwa: 21/03/2022