Swali: Ipi hukumu kwa wale wajitoa muhanga? Je, wanachukuliwa ni katika mashahidi?

Jibu: Kujitoa muhanga ili iwe shahaadah kwanza yatakikana iwe katika njia ya Allaah na si kwa ajili ardhi. Jambo la pili yatakikana iwe chini ya uongozi wa Kiislamu ukiongozwa na mtawala wa Waislamu. Ama hii milipuko iliopo leo, ni kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth iliopita:

“Hakika si venginevyo vitendo vinategemea na nia na kila mmoja ataliopwa kwa mujibu wa kile alichokusudia. Kwa hivyo yule aliyehama kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, basi uhamaji wake ni kwa ajili ya Allaah na Mtume wake, na yule ambaye uhamaji wake ulikuwa ni kwa ajili ya manufaa ya kidunia au kwa ajili ya kumuoa mwanamke fulani, basi uhamaji wake ulikuwa kwa kile kilichomuhamisha.”

Kwa kifupi ni kuwa milipuko hii sionelei kuwa inajuzu ila chini ya uongozi wa Kiislamu. Tukichukulia kuwa mtu kafanya kabisa kwa ajili ya Allaah (Ta´ala) atalipwa kwa nia yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: As’ilah wa Fataawa al-Imaaraat (2)
  • Imechapishwa: 09/04/2022