Swali: Katika mji wetu kuna kundi la Mashaykh wanaojinasibisha na madhehebu ya Ahl-us-Sunnah, pamoja na hivyo wanasema imani inazidi na kushuka kisha wanasema matendo ya viungo ni sharti ya kukamilika kwa imani. Ikiwa mtu hafanyi jema katu yuko mtu huyu chini ya matakwa ya Allaah maadamu anatamka Laa ilaaha illa Allaah…

Jibu: Huu ni upotofu. Huu ni upotofu. Akiacha matendo kwa kukusudia haitomfaa kitu laa ilaaha illa Allaah, kwa kuwa laa ilaaha illa Allaah ina Muqtadhwa wake na maana yake. Na ndio maana alipoambiwa Wahb bin Munabbih (Rahimahu Allaah):

“Je funguo ya Pepo si laa ilaaha illa Allaah?”

Akasema:

“Ndio, lakini hakuna funguo ila inakuwa na meno. Ukija na funguo yenye meno utafunguliwa. La sivyo hutofunguliwa.”

Meno anakusudia kuwa ni matendo. Laa ilaaha illa Allaah ni lazima kufanyia kazi Muqtadhwa wake na kufanyia kazi kwa alioyaweka Allaah katika Shari´ah na kuyafaradhisha kwa waja Wake. La sivyo nini itakufaidisha laa ilaaha illa Allaah kwa kutamka tu?

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://alfawzan.ws/sites/default/files/tg–1431-11-19.mp3 Tarehe: 1431-11-19/2010-10-26
  • Imechapishwa: 09/04/2022