Swali: Je, inafaa ikiwa nitahudhuria mimi na mke wangu na ndugu yangu wa kiume na mke wake katika kikao kimoja?
Jibu: Hakuna ubaya familia kukusanyika katika kikao kimoja, lakini kwa kuwepo kwa Hijaab na kujisitiri na kujiepusha na yale aliyoyaharamisha Allaah. Mwanamke ambaye ni mke wa ndugu yako wa kiume akiwa kwenu, mke wa mjomba wako, mke wa ami yako au mfano wa hayo akiwa nanyi katika kikao au nyumbani, basi hapana tatizo katika hilo. Hili limekuwepo tangu zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hadi leo. Watu hutembeleana, hutembeleana wao kwa wao na mtu asiye jamaa hutembelea nchi ya marafiki zake na nyumba za marafiki zake, hata kama si ndugu. Wanawake wao wanakuwa pamoja na wanawake wao na huenda wakakusanyika wote, lakini kwa Hijaab na kujisitiri. Sambamba na hayo kujiepusha na maneno machafu yasiyofaa. Yote haya hayana ubaya.
Swali: Vipi ikiwa hakuna Hijaab?
Jibu: Haijuzu. Ni wajibu kwake kujisitiri. Vinginevyo ajitenge na asikae nao. Ikiwa ni lazima akae, basi yule asiye Mahram kwake asimame au ainamishe macho yake na ajiepushe naye, ili awe ametekeleza amri ya Allaah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1736/حكم-اجتماع-الاخوين-مع-زوجتيهما-في-مجلس-واحد
- Imechapishwa: 03/07/2026
Swali: Je, inafaa ikiwa nitahudhuria mimi na mke wangu na ndugu yangu wa kiume na mke wake katika kikao kimoja?
Jibu: Hakuna ubaya familia kukusanyika katika kikao kimoja, lakini kwa kuwepo kwa Hijaab na kujisitiri na kujiepusha na yale aliyoyaharamisha Allaah. Mwanamke ambaye ni mke wa ndugu yako wa kiume akiwa kwenu, mke wa mjomba wako, mke wa ami yako au mfano wa hayo akiwa nanyi katika kikao au nyumbani, basi hapana tatizo katika hilo. Hili limekuwepo tangu zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hadi leo. Watu hutembeleana, hutembeleana wao kwa wao na mtu asiye jamaa hutembelea nchi ya marafiki zake na nyumba za marafiki zake, hata kama si ndugu. Wanawake wao wanakuwa pamoja na wanawake wao na huenda wakakusanyika wote, lakini kwa Hijaab na kujisitiri. Sambamba na hayo kujiepusha na maneno machafu yasiyofaa. Yote haya hayana ubaya.
Swali: Vipi ikiwa hakuna Hijaab?
Jibu: Haijuzu. Ni wajibu kwake kujisitiri. Vinginevyo ajitenge na asikae nao. Ikiwa ni lazima akae, basi yule asiye Mahram kwake asimame au ainamishe macho yake na ajiepushe naye, ili awe ametekeleza amri ya Allaah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1736/حكم-اجتماع-الاخوين-مع-زوجتيهما-في-مجلس-واحد
Imechapishwa: 03/07/2026
https://firqatunnajia.com/wanandugu-na-wake-zao-kukaa-kikao-kimoja/