Kinachowapasa wanazuoni juu ya Suufiyyah

Suufiyyah wana mambo ya ajabu na ya kushangaza miongoni mwa aina za shirki, upotofu, Bid´ah na maasi. Kwa hivyo inapaswa kuchunga na kujihadhari na shari yao na kujihadhari na yale waliyonayo miongoni mwa batili.

Ni wajibu kwa wanazuoni kuwaeleza watu hali yao na kwamba kila kundi katika nchi yoyote ile ni lazima hali yake ifafanuliwe na wanazuoni wa haki. Ni lazima pia waelezwe yale waliyonayo miongoni mwa batili, wafanyiwe majadiliano ya kielimu, wanazuoni wajitahidi mpaka wawabainishie haki na mpaka wawatoe katika yale waliyo ndani yake miongoni mwa batili.

Haya ni makundi mengi yaliyopo Shaam, ´Iraaq, Afrika, Misr na katika nchi nyingi. Inawapasa kwa wanazuoni walioko huko na kila anayeweza kufikia njia ya kuyajua kwa undani yale waliyonayo miongoni mwa batili ayabainishe kwa undani, jambo hili linahitaji kujifunza hali zao na kusimama juu ya yale waliyonayo miongoni mwa batili kwa ufafanuzi, kisha kuyabainisha hayo kwa maandishi, katika magazeti na majarida ili batili ibainike na haki iwe wazi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1760/خرافات-وشركيات-صوفية
  • Imechapishwa: 03/07/2026