Swali: Ameacha Twawaaf ya kuaga kwa ujinga?
Jibu: Inamlazimu arudi akafanye Twawaaf ya kuaga au achinje kondoo mmoja huko Makkah awape maskini na mafakiri, kwa sababu ya kuacha wajibu. Kwani Twawaaf ya kuaga ni miongoni mwa mambo ya wajibu ya Hajj. Akiacha wajibu huu, ima arudi atekeleza na hilo linatosha – Allaah akitaka – kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi, au atatoa fidia kwa kuchinja huko Makkah kwa sababu ya kuacha Twawaaf ya kuaga, basi hilo pia linatosha. Ni kama ilivyo kwa yule aliyeacha kurusha vijiwe kwenye kiguzo kisha akachinja damu, hilo humtosheleza. Lakini haifai kuacha kwa makusudi, haifai kuacha kwa makusudi. Anapata dhambi akiacha kwa makusudi kurusha vijiwe, akiacha baadhi yake au akaacha Twawaaf ya kuaga. Hilo halifai na atakuwa ametenda dhambi. Lakini akifanya hivyo na wakati ukapita, basi anawajibika kutoa damu. Vivyo hivyo akiacha Twawaaf ya kuaga kwa makusudi atakuwa ametenda dhambi, au akiacha kwa ujinga au kwa kusahau, basi arudi kutekeleza, au atoe fidia kwa kuchinja kondoo mmoja wa mbuzi aliyekamilisha mwaka mmoja, au wa kondoo aliyekamilisha miezi sita, kama ilivyo kwa Udhhiyah.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1778/حكم-من-ترك-طواف-الوداع-جاهلا
- Imechapishwa: 03/07/2026
Swali: Ameacha Twawaaf ya kuaga kwa ujinga?
Jibu: Inamlazimu arudi akafanye Twawaaf ya kuaga au achinje kondoo mmoja huko Makkah awape maskini na mafakiri, kwa sababu ya kuacha wajibu. Kwani Twawaaf ya kuaga ni miongoni mwa mambo ya wajibu ya Hajj. Akiacha wajibu huu, ima arudi atekeleza na hilo linatosha – Allaah akitaka – kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi, au atatoa fidia kwa kuchinja huko Makkah kwa sababu ya kuacha Twawaaf ya kuaga, basi hilo pia linatosha. Ni kama ilivyo kwa yule aliyeacha kurusha vijiwe kwenye kiguzo kisha akachinja damu, hilo humtosheleza. Lakini haifai kuacha kwa makusudi, haifai kuacha kwa makusudi. Anapata dhambi akiacha kwa makusudi kurusha vijiwe, akiacha baadhi yake au akaacha Twawaaf ya kuaga. Hilo halifai na atakuwa ametenda dhambi. Lakini akifanya hivyo na wakati ukapita, basi anawajibika kutoa damu. Vivyo hivyo akiacha Twawaaf ya kuaga kwa makusudi atakuwa ametenda dhambi, au akiacha kwa ujinga au kwa kusahau, basi arudi kutekeleza, au atoe fidia kwa kuchinja kondoo mmoja wa mbuzi aliyekamilisha mwaka mmoja, au wa kondoo aliyekamilisha miezi sita, kama ilivyo kwa Udhhiyah.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1778/حكم-من-ترك-طواف-الوداع-جاهلا
Imechapishwa: 03/07/2026
https://firqatunnajia.com/ameacha-twawaaf-ul-wadaa-kwa-ujinga/