Swali: Nimeanza kuswali swalah ya kujitolea, kisha ikaanza swalah ya faradhi. Je, aikate swalah yake au aimalizie?
Jibu: Sunnah ni kwamba aikate swalah hiyo ili aelekee kuswali faradhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ikikimiwa swalah, basi hakuna swalah isipokuwa ile ya faradhi.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Kwa hiyo ikianza swalah na yeye bado anaswali, basi aikate swalah hiyo na aingie pamoja na imamu ili ajitayarishe kuipata Takbiyr ya mwanzo.
Lakini ikiwa tayari ameshafanya Rukuu´ ya pili, basi hakuna kilichobaki. Ikiwa ataimalizia, swalah itakuwaimekwisha. Ikiwa yuko baada ya Rukuu´ ya pili au katika sijda ya mwisho, hakuna kinachomzuia kuimalizia, kwa sababu swalah hiyo tayari inakuwa imefikia mwisho.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1794/مشروعية-قطع-صلاة-النافلة-عند-اقامة-الصلاة-للفريضة
- Imechapishwa: 03/07/2026
Swali: Nimeanza kuswali swalah ya kujitolea, kisha ikaanza swalah ya faradhi. Je, aikate swalah yake au aimalizie?
Jibu: Sunnah ni kwamba aikate swalah hiyo ili aelekee kuswali faradhi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Ikikimiwa swalah, basi hakuna swalah isipokuwa ile ya faradhi.”
Ameipokea Muslim katika ”as-Swahiyh” yake.
Kwa hiyo ikianza swalah na yeye bado anaswali, basi aikate swalah hiyo na aingie pamoja na imamu ili ajitayarishe kuipata Takbiyr ya mwanzo.
Lakini ikiwa tayari ameshafanya Rukuu´ ya pili, basi hakuna kilichobaki. Ikiwa ataimalizia, swalah itakuwaimekwisha. Ikiwa yuko baada ya Rukuu´ ya pili au katika sijda ya mwisho, hakuna kinachomzuia kuimalizia, kwa sababu swalah hiyo tayari inakuwa imefikia mwisho.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1794/مشروعية-قطع-صلاة-النافلة-عند-اقامة-الصلاة-للفريضة
Imechapishwa: 03/07/2026
https://firqatunnajia.com/kata-swalah-ya-kujitolea-na-ujiunge-na-swalah-ya-faradhi/