Swali 237: Je, inajuzu kuswali Rak´ah mbili wakati ninapoingia msikitini na Khatwiyb anakhutubu siku ya ijumaa? Kwa sababu watu wengi wananikataza kuswali wakati Khatwiyb anakhutubu?

Jibu: Mimi nakutajia Hadiyth ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa sababu masuala haya wanachuoni wa Hadiyth wa Ahnaaf na wengineo wametofautiana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Anapoingia mmoja wenu msikitini basi asikae mpaka kwanza aswali Rak´ah mbili.”

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kama ilivyotajwa katika “as-Swahiyh” kupitia kwa Jaabir ambapo alikuwa anatoa Khutbah juu ya mimbari siku ya ijumaa na akaingia mtu akawa ameketi. Akasema: “Je, umeswali Rak´ah mbili?” Akajibu: “Hapana”. Akasema: “Simama uswali Rak´ah mbili.”

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 458
  • Imechapishwa: 01/11/2019