Swali: Je, ni haramu kwangu kusoma ili niweze kupata vyeti/shahadah? Nifanye vipi ili masomo yangu yawe kwa ajili ya Allaah?

Jibu: Hili ni swali muhimu ambapo mtu anasoma ili aweze kupata vyeti. Tunamuuliza huyu muulizaji, je, unataka vyeti ili uweze kufikia cheo cha juu na ngazi ya kipesa? Basi nia hii imekhasirika. Au unataka kupata vyeti kwa sababu ya kufikia sehemu ambayo unaweza kuwanufaisha waislamu katika kufundisha, kuhukumu au kazi? Hii ni nia nzuri isiyopingana na Ikhlaasw. Kwa sababu tunajua kwamba hii leo ili uweze kupata nafasi ambayo utaweza kwayo kuwanufaisha watu inakuwa kupitia vyeti. Asiyekuwa na vyeti, japokuwa atakuwa ni miongoni mwa wajuzi zaidi katika watu, hawezi kupewa nafasi kwa mfano afundishe chuo kikuu au sekondari. Kwa hivyo ukitafuta elimu ili uweze kupata vyeti vitavyokuwezesha kufikia nafasi ya uongozi katika jamii – kama vile ualimu, hakimu, mudiri na mfano wa hayo – basi hii ni nia nzuri na haina madhambi ndani yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (58) http://binothaimeen.net/content/1321
  • Imechapishwa: 01/11/2019