Wanafunzi wanaochelea kuoa kwa ajili ya ufakiri

Swali: Baadhi ya wanafunzi na walinganizi katika dini ya Allaah wanapoelekea kutafuta elimu wanachelea ufakiri na wanapofikiria kuoa wanaacha na kusema ni nini atachompa mwanamke huyu na kumhudumia. Je, kitendo hichi kinazingatiwa ni katika shirki kwenye Rubuubiyyah na Allaah ndiye Muumbaji na Mwenye kuruzuku na kwamba hakufanyia kazi muqtadha hii?

Jibu: Ni upungufu na sio shirki. Ni upungufu katika Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah. Lililo la wajibu ni yeye kumtegemea Allaah. Kumtegemea Allaah ni katika Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah. Kutegemea ni katika ´ibaadah:

فَاعْبُدْهُ وَتَوَكَّلْ عَلَيْهِ

“Mwabudu na mtegemee Yeye.” (11:123)

Lililo la wajibu ni yeye kumtegemea Allaah.

Kuhusu yeye kuoa hili ni jambo linalorejea kwake; akitaka kuoa ataoa na asipotaka ataacha. Itategemea na hali ya maisha yake na uwezo wake:

وَلْيَسْتَعْفِفِ الَّذِينَ لَا يَجِدُونَ نِكَاحًا حَتَّىٰ يُغْنِيَهُمُ اللَّـهُ مِن فَضْلِهِ

“Wajizuilie na machafu ambao hawana uwezo wa ndoa mpaka Allaah awatajirishe katika fadhilah Zake.” (24:33)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (38) http://alfawzan.af.org.sa/node/2146
  • Imechapishwa: 13/07/2020