Swali: Vitabu vya dini ghali kama tafsiri ya Qur-aan ya Ibn Kathiyr, “as-Swahiyh” ya al-Bukhaariy na ya Muslim. Vijana watajifunza vipi dini yao?
Jibu: Kusema kwamba viko ghali uhakika wa mambo ni kuwa jambo linatofautiana kwa kutegemea na miji na hali za watu. Lakini vitabu vipo kwenye maktabah za vitabu. Kijana mwenye pupa anaweza kwenda maktabah yoyote na akapata kile anachokitaka. Ikiwa kwenye mji wake hakuna maktabah tunazokusudia kama anaweza kununua basi anunue. Vinginevyo inafaa kupewa zakaah anunue vitabu hivi anavyohitajia katika dini yake.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (10) http://binothaimeen.net/content/6736
- Imechapishwa: 15/11/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)