Swali: Baadhi ya watu wanasema kuwa siku ya ijumaa ni siku nzito na watu wanachoshwa nayo, pamoja na kukubali fadhila na ubora wake. Ni ipi hukumu ya hisia hii?

Jibu: Hii ni sifa ya wanafiki. Wao ndio wanaonelea kuwa siku ya ijumaa ni siku nzito na wanaonelea kuwa swalah ni nzito na wanasimama kwa uvivu wakati wa swalah. Kusema mfano wa maneno haya haijuzu na tunaomba kinga kwa Allaah. Siku ya ijumaa sio siku ngumu. Ijumaa ni siku yenye fadhila. Siku yenye raha kwa watu waumini na ngumu kwa wanafiki.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-5-29.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014