Mgonjwa kufupisha swalah za Rak´ah nne

Swali: Inajuzu kwa mgonjwa kufupisha swalah za Rak´ah nne?

Jibu: Hapana. Kufupisha inakuwa maalum katika safari. Inajuzu kwa mgonjwa kujumuisha tu. Hapa hukosea baadhi ya watu wa kawaida ambao hudhania kujumuisha kunalazimisha kufupisha. Hivyo wanafupisha. Hili halijuzu. Mkazi hafupishi, ni mamoja ikiwa ni mtu mgonjwa au aliye na afya. Bali baadhi ya maimamu wa misikiti wanapojumuisha kwa ajili ya mvua wanafupisha swalah ya ´Ishaa. Hili ni kosa kubwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Zaad-il-Ma´aad (08) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/mo–1430-10-15.mp3
  • Imechapishwa: 15/11/2014