Swali: Una nasaha zozote kwa ambaye anaswali Fajr baada ya kutoka wakati wake anaswali pale anapotaka kwenda kazini?
Jibu: Hili ni tendo la jinai kubwa kwa yeye kuswali Fajr wakati anapoenda kazini. Kuna kikosi cha wanachuoni ambacho kimetoa fatwa kwamba anakuwa mwenye kuritadi akiwa na mazowea ya kufanya hivo. Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) ametoa fatwa hiyo na jopo la wanachuoni wengine. Kwa sababu hakutekeleza swalah ndani ya wakati wake. Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]
Yule ambaye anaweka alamu ya saa juu ya kazi yake na anaamka pale ambapo umefika wakati wa kwenda kazini kwake, basi itambulike kuwa kuna kikosi cha wanachuoni ambacho kimetoa fatwa kuwa anakuwa murtadi. Wapo wanachuoni wengine waliosema kuwa dhambi yake ni kubwa zaidi kuliko dhambi ya mzinifu, mwizi na mnywaji pombe ijapo hawi kafiri aliyekufuru kufuru kubwa. Kuhusu yule ambaye imempita pasi na kukusudia ni mwenye kupewa udhuru.
[1] 04:103
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
- Imechapishwa: 14/06/2020
Swali: Una nasaha zozote kwa ambaye anaswali Fajr baada ya kutoka wakati wake anaswali pale anapotaka kwenda kazini?
Jibu: Hili ni tendo la jinai kubwa kwa yeye kuswali Fajr wakati anapoenda kazini. Kuna kikosi cha wanachuoni ambacho kimetoa fatwa kwamba anakuwa mwenye kuritadi akiwa na mazowea ya kufanya hivo. Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) ametoa fatwa hiyo na jopo la wanachuoni wengine. Kwa sababu hakutekeleza swalah ndani ya wakati wake. Allaah (Ta´ala) amesema:
إِنَّ الصَّلَاةَ كَانَتْ عَلَى الْمُؤْمِنِينَ كِتَابًا مَّوْقُوتًا
“Kwani hakika swalah kwa waumini ni fardhi iliyowekwa nyakati maalum.”[1]
Yule ambaye anaweka alamu ya saa juu ya kazi yake na anaamka pale ambapo umefika wakati wa kwenda kazini kwake, basi itambulike kuwa kuna kikosi cha wanachuoni ambacho kimetoa fatwa kuwa anakuwa murtadi. Wapo wanachuoni wengine waliosema kuwa dhambi yake ni kubwa zaidi kuliko dhambi ya mzinifu, mwizi na mnywaji pombe ijapo hawi kafiri aliyekufuru kufuru kubwa. Kuhusu yule ambaye imempita pasi na kukusudia ni mwenye kupewa udhuru.
[1] 04:103
Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (14)
Imechapishwa: 14/06/2020
https://firqatunnajia.com/wanachuoni-wamefutu-kwamba-mtu-aina-hii-ni-kafiri/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)