Swali: Baadhi ya watu wanataka mtu aache kiwango kikubwa cha Sunnah zilizothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kwa kujengea hoja kwa Hadiyth mfano wa:
“Ee ´Aaishah! Lau kama si watu wako ndio punde wametoka katika ukafiri, basi ningeliijenga Ka´bah kutokana na misingi ya Ibraahiym na kuifanya kuwa na milango miwili; mlango mmoja watu wanaingia na mlango mwingine watu wanatokea.”[1]
Vilevile wanatumia hoja kwa yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuacha kuwaua wanafiki wanaotambulika na kuacha kuyavunja masanamu Makkah kabla ya yeye kuhajiri. Ni vipi kuraddi hoja tata hii?
Jibu: Aliyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni haki. Sisi tunamuigiliza Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
وَمَا يَنطِقُ عَنِ الْهَوَىٰ إِنْ هُوَ إِلَّا وَحْيٌ يُوحَىٰ
”Hatamki kwa matamanio yake. Hayo ayasemayo si chochote isipokuwa ni Wahy unaofunuliwa kwake.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Yale ninayokukatazeni yaepukeni na yale ninayokuamrisheni yafanyeni muwezavyo.”[3]
وَمَا آتَاكُمُ الرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَاكُمْ عَنْهُ فَانتَهُوا ۚ وَاتَّقُوا اللَّـهَ ۖ إِنَّ اللَّـهَ شَدِيدُ الْعِقَابِ
”Kile anachokupeni Mtume, basi kichukueni, na kile anachokukatazeni, basi kiacheni. Mcheni Allaah; hakika Allaah ni mkali wa kuadhibu.”[4]
Lakini kwa sababu tu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliacha kuiboresha Ka´bah kutokana na misingi ya Ibraahiym, haifahamishi kwamba tuzue fujo katika dini ya Allaah. Je, tule mirungi kwa sababu tu watu wanakula mirungi? Tuvute sigara kwa sababu tu watu wanavuta sigara? Kama wamejiunga vyamavyama, nasi tujiunge pamoja nao? Wanachotaka kwa hoja tata hizi ni kututenganisha mbali na Qur-aan na Sunnah – vinginevyo ni kututuhumu kuwa na misimamo mikali, kuchupa mipaka, Wahhaabiy na kadhalika. Mimi nakwambia wewe na muulizaji ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikubaliwa na Mola wake. Allaah (Subhanaahu wa Ta´ala) amesema:
فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا
“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.”[5]
Allaah amemlinda Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), lakini mimi na wewe tunapatia na kukosea, tunajua na hatujui. Haitakiwi kwetu kuleta fujo katika dini ya Allaah:
لَيْسَ لَكَ مِنَ الْأَمْرِ شَيْءٌ أَوْ يَتُوبَ عَلَيْهِمْ أَوْ يُعَذِّبَهُمْ فَإِنَّهُمْ ظَالِمُونَ
”Si juu yako katika amri kuamua lolote; ima awasamehe au awaadhibu, kwani wao ni madhalimu.”[6]
Kwa hivyo ikiwa mtu anataka kuwaua wanafiki, tutamwambia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuwaua wanafiki, na kama mtu atataka kuboresha Ka´bah kutokana na misingi ya Ibraahiym, tutamwambia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakufanya hivo. Vivyo hivyo ndivo tutasema juu ya yale mengine yote ambayo yaliachwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
[1] al-Bukhaariy (126).
[2] 53:3-4
[3] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).
[4] 59:7
[5] 4:65
[6] 3:128
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 400-401
- Imechapishwa: 21/01/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 400-401
Imechapishwa: 21/01/2025
https://firqatunnajia.com/wanachotaka-ni-kututenganisha-na-qur-aan-na-sunnah-vinginevyo-tuna-msimamo-mkali/