Swali: Ikiwa mimi nilinyonya kutoka kwa mwanamke, je, watoto wa mume wake kutoka kwa wake wengine ni ndugu zangu?
Jibu: Ndiyo, ikiwa umenyonyeshwa na mke wa Zayd, Faatwimah, akakunyonyesha kutokana na maziwa ya mume wake naye akiwa pamoja naye, kunyonyeshwa kamili kusikopungua mara tano na wewe ukiwa ndani ya miaka miwili, kabla ya kuachishwa ziwa, basi unakuwa mtoto wake na mtoto wa mume wake. Unakuwa ndugu kwa watoto wake kutoka kwa mume wa zamani au mume wa baadaye. Na pia unakuwa ndugu kwa watoto wa huyu mume kutoka kwa wake waliotangulia na waliokuja baadaye, ndugu kwa upande wa baba kwa kunyonyeshwa. Unakuwa ndugu kwa watoto wake na huyu mwanamke, ndugu wa pamoja kwa kunyonyeshwa. Unakuwa ndugu kwa watoto wake ikiwa ana watoto kutoka kwa mume wa zamani, ndugu kwa upande wa mama kwa kunyonyeshwa. Ni kama nasaba, huharamishwa kwa kunyonyeshwa yale yanayoharamishwa kwa nasaba.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3234/الابناء-اخوة-لمن-رضع-من-زوجة-ابيهم
- Imechapishwa: 02/08/2026
Swali: Ikiwa mimi nilinyonya kutoka kwa mwanamke, je, watoto wa mume wake kutoka kwa wake wengine ni ndugu zangu?
Jibu: Ndiyo, ikiwa umenyonyeshwa na mke wa Zayd, Faatwimah, akakunyonyesha kutokana na maziwa ya mume wake naye akiwa pamoja naye, kunyonyeshwa kamili kusikopungua mara tano na wewe ukiwa ndani ya miaka miwili, kabla ya kuachishwa ziwa, basi unakuwa mtoto wake na mtoto wa mume wake. Unakuwa ndugu kwa watoto wake kutoka kwa mume wa zamani au mume wa baadaye. Na pia unakuwa ndugu kwa watoto wa huyu mume kutoka kwa wake waliotangulia na waliokuja baadaye, ndugu kwa upande wa baba kwa kunyonyeshwa. Unakuwa ndugu kwa watoto wake na huyu mwanamke, ndugu wa pamoja kwa kunyonyeshwa. Unakuwa ndugu kwa watoto wake ikiwa ana watoto kutoka kwa mume wa zamani, ndugu kwa upande wa mama kwa kunyonyeshwa. Ni kama nasaba, huharamishwa kwa kunyonyeshwa yale yanayoharamishwa kwa nasaba.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3234/الابناء-اخوة-لمن-رضع-من-زوجة-ابيهم
Imechapishwa: 02/08/2026
https://firqatunnajia.com/wana-hao-ni-ndugu-wa-wale-walionyonyeshwa-na-mke-wa-baba-yao/