Wametenga sehemu ya kuswalia nyumbani na kuacha kwenda msikiti wanaosikia adhaana

Swali: Sisi ni kundi la wasudan tumechukua nyumba kwa ajili ya kutatua baadhi ya masuala. Kuna baadhi ya ndugu wameifanya nyumba hii makazi yao. Kwa kuwa nyumba ni pana sana na idadi ni kubwa karibu watu ishirini kwa wakati mmoja, tumechukua sehemu ya nyumba hii kama msikiti na imewekewa mazulia kwa ajili ya kuswali, kwa sababu misikiti uko mbali kidogo na inatutenganisha nayo barabara za haraka na zenye msongamano, hali ya kuwa tunasikia adhaana katika misikiti hiyo. Sisi tunaadhini katika nyumba hii na tunasimamisha swalah. Je, inasihi?

Jibu: Haijuzu kwenu kuswali nyumbani. Amesema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yeyote mwenye kusikia wito na asiitikie, basi hakuna swalah kwake isipokuwa kwa udhuru.”

Isipokuwa ikiwa misikiti iko mbali nanyi umbali unaofanya kuhudhuria swalah baada ya adhaana kuwa ni jambo gumu, basi huu ni udhuru. Lakini muda wa kuwa mnasikia adhaana ya kawaida bila kipaza sauti – ama kipaza sauti hufikisha sauti kutoka mbali – lakini ikiwa adhaana ingekuwa bila kipaza sauti mngesikia wakati wa utulivu wa sauti na kutokuwepo magari yanayochanganya, basi ni lazima juu yenu kuhudhuria. Ama ikiwa uko mbali kiasi kwamba mkiondoka baada ya adhaana hamfikii swalah kwa sababu ya umbali wake na mnasikia sauti kwa sababu ya kipaza sauti tu na si kwamba uko karibu, basi huu ni udhuru kwenu. Muumini anapaswa kujihesabu nafsi yake mwenyewe. Ni juu yake kumcha Allaah. Ikiwa mnaweza kuhudhuria misikitini, basi ni wajibu kuhudhuria misikitini. Ikiwa uko mbali nanyi kiasi kwamba haiwezekani kwenu kuhudhuria baada ya adhaana kwa sababu ya wingi wa barabara na umbali wake mpaka swalah inapita, basi huu ni udhuru kwenu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3488/حكم-الصلاة-في-البيت-بسبب-بعد-المسجد
  • Imechapishwa: 30/08/2026