Inapendekezwa kuwa kusoma Qur-aan kuwe katika mahali safi na palipochaguliwa. Kwa sababu hiyo wanazuoni wengi wamependelea kusoma ndani ya msikiti kwa kuwa unakusanya usafi, utukufu wa mahali na kupata fadhilah nyingine ambayo ni I´tikaaf. Kwani inapasa kwa kila anayekaa msikitini awe na nia ya I´tikaaf, ni mamoja iwe anakaa muda mrefu au mfupi. Bali inapasa anapoingia msikitini mara ya kwanza awe na nia ya I´tikaaf. Adabu hii inapaswa kuzingatiwa, kuenezwa na kufundishwa kwa watoto na watu wa kawaida, kwani ni katika mambo yanayopuuzwa mara nyingi.
Ama kusoma ndani ya bafu, wanazuoni wa mwanzo wametofautiana kuhusu kuchukiza kwake. Wafuasi wetu wamesema kuwa haichukizi, jambo ambalo limenukuliwa na Imaam mwenye hadhi kubwa, Abu Bakr bin al-Mundhir katika “al-Ishraaf” kutoka kwa Ibraahiym an-Nakha´iy na Maalik. Hayo pia ndio maoni ya ´Atwaa.
Makundi mengine yameona kuwa inachukizi. Miongoni mwao ni ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). Hayo yamepokewa na Ibn Abiy Daawuud kutoka kwake. Ibn-ul-Mundhir amenukuu maoni hayohayo kutoka kwa kikosi cha wanafunzi wa Maswahabah. Miongoni mwao Abu Waa-il Shaqiyq bin Salamah, ash-Sha´biy, al-Hasan al-Baswriy, Mak-huul na Qabiyswah bin Dhu´ayb. Tumeyapokea maoni hayohayo pia kutoka kwa Ibraahiym an-Nakha´iy. Wafuasi wetu wameyanukuu kutoka kwa Abu Haniyfah – Allaah awe radhi nao wote! ash-Sha´biy amesema:
”Kusoma Qur-aan kunachukizwa katika sehemu tatu: ndani ya mabafu, vyooni na katika nyumba za mashine za kusaga zinapokuwa zinafanya kazi.”
Abu Maysarah amesema:
”Allaah hatajwi isipokuwa katika mahali pazuri.”
Kuhusu kusoma Qur-aan njiani, maoni yaliyochaguliwa ni kuwa inajuzu na haichukizi ikiwa msomaji hatashughulishwa. Ikiwa atashughulika basi inachukizwa, kama alivyochukia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kusoma kwa mwenye usingizi kwa kukhofia kuchanganya. Abu Daawuud amepokea kutoka kwa Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) ya kwamba alikuwa akisoma Qur-aan njiani na kwamba ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) ameruhusu kitendo hicho. Ibn Abiy Daawuud amesema: Abur-Rabiy´ amenihadithia: Ibn Wahb ametukhabarisha:
”Nilimuuliza Maalik kuhusu mtu anayeswali usiku mwishoni, kisha anatoka kwenda msikitini huku bado amebakiwa na sehemu ya Suurah aliyokuwa akisoma? Akasema: ”Sijui kama kusoma Qur-aan kunafaa kufanywa njiani.” Akachukizwa na jambo hilo.”
Hii ni cheni ya wapokezi Swahiyh kutoka kwa Maalik (Rahimahu Allaah).
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 51-53
- Imechapishwa: 30/08/2026

Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 51-53
Imechapishwa: 30/08/2026
https://firqatunnajia.com/44-mahali-pa-kusoma-qur-aan/