1Bwana ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako?

Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu?

2Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki,

asemaye kweli toka moyoni mwake,

3Na hana masingizio ulimini mwake,

asiyemtenda jirani yake vibaya,

na asiyemsingizia mwenzake,

4 Ambaye humdharau mtu mbaya,

lakini huwaheshimu wale wamwogopaoa Bwana,

yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia.

5 Yeye akopeshaye fedha yake bila ribaa,

na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.

Mtu afanyaye haya kamwe hatatikisika.

  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Zaburi 15:01
  • Imechapishwa: 16/01/2020