Wakati unataka kuosha mkojo kwenye nguo au mwilini lakini hujui ni wapi

Swali: Afanye nini ikiwa mtu ana mkojo mwilini mwake lakini hajui ulipo?

Jibu: Atajitahidi kuosha pale anapodhani umeingia. Atajitahidi ni wapi ambapo mkojo unaweza kuwa mwilini mwake au kwenye nguo zake na aoshe sehemu hiyo. Ikiwa hawezi hilo, basi aoshwe nguo nzima.

Swali: Je, inatosha kunyunyizia maji?

Jibu: Hapana, kama ni mkojo haitosh kurashia kwa maji. Kunyunyuza maji kunafaa wakati inapokuwa ni madhiy na mkojo wa mtoto wa kiume ambaye hajaanza kula chakula cha kawaida.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24712/حكم-من-اصابه-بول-لا-يعلم-موضعه
  • Imechapishwa: 30/11/2024