Swali: Je, mtu inafaa kwa mtu kuitikia adhaana akiwa chooni?

Jibu: Hapana, asimuitikie.

Swali: Je, inafaa kumuitikia baada ya kutoka chooni?

Jibu: Baadhi ya wanazuoni wanaona kuwa anaweza kulipa, lakini hakuna dalili ya wazi ya hilo.

Swali: Vipi ikiwa ataitikia adhaana kwa moyo wake tu?

Jibu: Kujibu kwa moyo hakuna tatizo, popote pale alipo. Hata hivyo haizingatiwi kuwa ni kuitikia adhaana.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24709/هل-يقضي-ترديد-الاذان-من-سمعه-في-الخلاء
  • Imechapishwa: 30/11/2024