Swali: Nini maana ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Hakika si venginevyo kilichowaangamiza waliokuwa kabla yenu ni maswali yao mengi.”?

Jibu: Wanachupa mpaka. Walikuwa wanawauliza Mitume wao hali ya kujikakama kisha wanatofautiana nao. Mtu haulizi isipokuwa wakati anapohitajia haja ya kielimu. Ama kuchupa mpaka haifai. Kwa ajili hiyo amesema (Jalla wa ´Alaa):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَسْأَلُوا عَنْ أَشْيَاءَ إِن تُبْدَ لَكُمْ تَسُؤْكُمْ

“Enyi mlioamini! Msiulizie mambo ambayo mkidhihirishiwa yatakuchukizeni.” (05:101)

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21506/معنى-انما-اهلك-من-كان-قبلكم-كثرة-سوالهم
  • Imechapishwa: 24/08/2022