Wajibu juu ya nduguyo ambaye ameanza kupinda

Swali: Mimi nina ndugu ambaye nampenda kwa ajili ya Allaah. Lakini ndugu huyu ameanza kujitenga mbali kukaa na watu wema pamoja vilevile na kuzembea katika upande wa matendo mema na ´ibaadah na kulemea katika dunia. Vilevile kutumbukia katika baadhi ya maasi. Kwa ajili hiyo naomba umpe nasaha kijana huyu na wengineo waliopondoka kutoka katika njia hii?

Jibu: Namuomba atuongoze sisi na yeye. Ni lazima kwako kumnasihi amche Allaah (´Azza wa Jall), achunge haki za Tawhiyd na imani na kutekeleza mambo ya wajibu. Sambamba na hilo ajiepushe na mambo ya haramu, alazimiane na matendo mema na atahadhari kutokamana na maasi. Wakati mwingine  Allaah anaweza kumfanyia njama mtu. Maasi yanaweza kuwa ni sababu ya kupata mwisho mbaya. Ni wajibu kwake kumcha Allaah na atahadhari, ahifadhi yale ambayo Allaah amemuwajibishia na ayaepuke yale Allaah aliyomuharamishia. Vilevile ni  wajibu kwako kumuombea du´aa na uwaombe baadhi ya wanafunzi waongee nae. Huenda Allaah akamwongoza. Huenda akarudi katika yale aliyokuwemo hapo kabla.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (07) http://dl.islamweb.net/audiopath/audio/lecturs/aalrrajhee/434/434.mp3
  • Imechapishwa: 22/12/2018