Wafanyakazi wa kike majumbani hii leo ni wamilikiwa?

Swali: Baadhi ya watu wanaona kuwa wafanyakazi wa kike wanaokuwa majumbani wanakuwa ni wenye kumilikiwa na yule baba mwenye nyumba.  Allaah amesema:

 وَمَا مَلَكَتْ أَيْمَانُكُمْ

“Na wale iliyowamiliki mikono yenu ya kulia.”[1]

Jibu: Imani hii si sahihi. Kuamini kwamba mfanyakazi wa kike ni mmilikiwa ni kosa kubwa. Mfanyakazi si mwenye kumilikiwa. Yuko huru. Si halali kwa mtu kutazama uso wake au kuzungumza naye pasi na haja. Kwa sababu ni ajinabi kwake. Lakini hapa kuna njia sahali: ikiwa mfanyakazi huyu bado ni kijana na hana mume, basi huyu baba mwenye nyumba amuoe ili awe mke wa pili ambaye atasaidizana na yule mke wa kwanza katika haki za nyumbani na amsaidie vilevile katika makazi ya nyumbani. Hili ni bora. Hapo mfanyakazi huyu atakuwa ni halali kwake kupitia njia ya ndoa.

[1] 04:36

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (45) http://binothaimeen.net/content/1049
  • Imechapishwa: 23/06/2020