Waalimu na wanafunzi wanapaswa kuwa viigizo vyema

Swali: Mimi ni mwalimu katika shule ya usiku na mkuu wa shule amechelewesha swalah ya ´Ishaa mpaka baada ya somo la tatu, ilihali somo la pili linaisha wakati wa adhaana ya ´Ishaa. Isitoshe karibu kuna msikiti mkubwa. Nifanye nini?

Jibu: Wajibu kwa waalimu na wanafunzi ni kuswali pamoja na mkusanyiko, kisha warudi kwenye masomo yao. Haifai kutanguliza somo juu ya swalah ya mkusanyiko. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha kuitikia adhaana:

”Yeyote anayesikia wito kisha asiitikie, basi hana swalah isipokuwa kwa udhuru.”

Waalimu ndio wa kwanza kuitikia na vivyo hivyo wanafunzi, kwani wao ni viongozi. Ni wajibu kuitikia mwito wa Allaah na kuchelewesha somo mpaka waswali kwanza.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3226/تاخير-صلاة-الجماعة-من-اجل-الدراسة
  • Imechapishwa: 02/08/2026