Vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah vilivopo kwenye maktabah ya msikitini

Swali: Je, inajuzu kuchukua vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah wadh-Dhwalaal na kuvichana kwenye maktbah ya msikitini pamoja na kujua kuwa ni maktbah ya jumla kwa watu wote wanaokuja kuswali?

Jibu: Hapana. Wewe humiliki hilo. Lakini hata hivyo ukiona vitabu vya Bid´ah na upotevu unachotakiwa ni kuzungumza na imamu wa msikitini ambaye ndiye msimamizi wa maktbah. Mzungumzishe yule mwenye usimamizi wa maktabah hiyo ili aondoshe vitabu hivo. Ama wewe humiliki hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/al_makruf-14-08-1433.mp3
  • Imechapishwa: 15/06/2015