Swali: Ni vitabu vipi unavyopendeza na ni vipi unavyotahadharisha? Ingelikuwa bora endapo ungetutajia baadhi ya majina ya vitabu hivyo.
Jibu: Napendekeza Qur-aan, Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na urithi wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kwa ujumla. Havihesabiki wala kudhibitiwa. Vinatosheleza kwa yule ambaye anataka kheri. Yule ambaye anataka marejeo juu ya dini na elimu yake hahitaji vitabu vya Ahl-ul-Bid´ah.
Tunatahadharisha vitabu vya wazushi na wapotofu kukiwemo vitabu vya Suufiyyah, vitabu vya Khawaarij, vitabu vya Raafidhwah, vitabu vya al-Ikhwaan al-Muslimuun na vitabu vya Qutbiyyuun. Vitabu vyote hivi vinahesabika ni vitabu vya Bid´ah na upotofu ambavyo tunawatahadharisha navyo vijana wa ummah. Vilevile kanda za watu sampuli hii ambao wanaenda kinyume na mfumo wa Salaf.
Yule ambaye Allaah anamtakia haki na kufuata mfumo wa Salaf basi vyanzo vyao vimejaa na ni vingi sana. Mtu anaweza kumaliza maisha yake yote na asimalize baadhi yake. Ni kipi basi kinachompelekea huko? Bali mwanzoni mwa kutafuta kwake elimu utamuona anaanza kutapatapa, kuyumbayumba na kukimbilia nyuma ya vitabu vya wapotofu na kusema kuwa eti anaweza kutofautisha ambapo akachukua haki na akaacha batili. Matokeo yake anachukua batili na kuiacha haki. Haya hutokea mara nyingi kama tulivyoashiria punde.
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Kashf-us-Sitaar, uk. 20
- Imechapishwa: 07/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)