Vitabu kuhusu fadhilah za Suurah mbalimbali

Swali: Imethibiti kuwa Suurah “al-Zalzalah”, “an-Naswr” na nyingezo kuzisoma ni sawa na robo ya Qur-aan. Je, hilo ni sahihi?

Jibu: Linahitajia uthibitisho. Aliyesema hivi ni juu yake athibitishe hilo. Kwa kuwa kuna uwongo mwingi juu ya fadhilah za Suurah. Kuna mmoja katika waongo ameweka fadhilah kwa kila Suurah kwa mujibu wake na akanasibisha hilo kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wakati alipoulizwa juu ya hilo akasema kuwa ni kwa sababu aliona watu wameipa mgongo Qur-aan na hivyo ndio akataka kuwavutia nayo! Shaytwaan ndio amemwambia hivi na akawa amefanya. Vitabu juu ya daraja ya Hadiyth vipo. Usikubali upokezi wowote isipokuwa baada ya kuukagua kutoka kwenye vitabu sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (22) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-7.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020