Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kutumia vipodozi vipya na vya kitamaduni na kujipodoa kwenye nywele na mwili wake na kujipamba mbele ya mumewe na wanawake wengine mbele ya masherehe?

Jibu: Nywele hazitakiwi kupakwa rangi nyeusi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Katika zama za mwisho watakuwepo watu wanaozipaka nywele rangi nyeusi kama kifua cha njiwa; hawatonusa harufu ya Peponi.”[1]

Ikiwa ni vipodozi vyengine visivyokuwa hivo, basi hapana vibaya akajipamba mbele ya mumewe au mbele ya wanawake wengine.

[1] al-Albaaniy amesema:

“Ameipokea Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ahmad, adh-Dhwiyaa’ al-Maqdisiy katika ”al-Mukhtaarah” na wengine wengi ambao hakuna nafasi ya kuwataja. Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh na kwa ni kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim.” (Ghaayat-ul-Maraam, uk. 70-71)

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 594
  • Imechapishwa: 05/06/2025