Swali: Nilimuuliza ndugu ´Aqiyl kuhusu maquillage [vipodozi], akanambia kuwa ni kujifananisha na makafiri pamoja na kujua kuwa Shaykh Ibn Baaz amesema kuwa inajuzu kwa mke. Ni yapi maoni yako? Je, vipodozi vinazuia wudhuu´ na khaswa al-Hamuurah inayopakwa kwenye midomo?

Jibu: Ukijiepusha nayo ni bora zaidi. La sivyo sionelei kuzuizi.

Kuhusu kwamba inazuia maji au haizuii, mimi sijawahi kugusa mwili uliyopaka vipodozi ili niweze kuangalia kama ni sahihi au si sahihi. Paka wewe au mwingine aweke vipodozi hivi vyekundu kisha aweke juu yake maji, akiona maji yamefika katika mwili na umelowa, itakuwa ni sawa, na ikiwa vinazuia, itakuwa haijuzu kuvitumia.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=2957
  • Imechapishwa: 03/05/2015