Vipi ikiwa mtu amekuja msikitini anataka kuswali Maghrib katika swalah ya ´Ishaa na amekuta mkusanyiko uko katika Rak’ah ya pili? Jibu ni kuwa ajiunge pamoja nao kwa nia ya Maghrib na atoe salamu pamoja na imamu. Hilo halidhuru. Kwa kuwa hukuzidisha na wala hukupunguza. Hili halina utata. Pamoja na hivyo linawachanganya baadhi ya watu. Wanasema ukijiunga nao katika Rak’ah ya pili kisha ukakaa Tashahhud ambapo kwa imamu ni Rak’ah ya pili na kwako inahesabika ni Rak’ah ya kwanza, si utakuwa umekaa Tashahhud katika Rak’ah ya kwanza? Jibu ni kuwa hili halidhuru. Kwa sababu wewe ukimkuta imamu katika Rak’ah ya pili katika swalah ya Dhuhr, imamu atakaa Tashahhud ya kwanza na wewe utakuwa uko katika Rak’ah ya kwanza. Sura hii ni sawa na ile ya kwanza. Hakuna kitu cha kuchanganya.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/387-388)
- Imechapishwa: 30/05/2023
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)