Vipi muislamu anavyojitibu kutokana na mahuzuniko na msongo wa mawazo?

Swali: Wakati mwingine mtu anapatwa na masononeko na msongo wa mawazo. Muislamu anajitibu vipi? Je, imesuniwa mtu akajifanyia matabano mwenyewe?

Jibu: Mosi mtu anapaswa kujua kuwa masononeko na msongo wa mawazo yanayompata mtu ni miongoni mwa yale mambo ambayo yanafuta na kuyapunguza madhambi ya mtu. Iwapo atafanya subira na kutaraji malipo basi analipwa thawabu kwa jambo hilo. Pamoja na hivyo hapana vibaya kwa mtu akaomba zile du´aa zilizopokelewa kwa ajili ya kuondosha masononeko na msongo wa mawazo. Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna mja anayesibiwa na majonzi na huzuni na kusema:

اللهُمَّ إِني عَبْدُكَ وابنُ عَبْدِكَ وابْنُ أَمتِكَ نَاصيتي بيَدِكَ ماضٍ فِيَّ حُكْمُكَ عَدْلٌ فيَّ قَضَاؤُكَ أَسْأَلُكَ بِكُلِّ اسْمٍ هُوَ لَكَ سَمَّيتَ بِهِ نَفْسَكَ أَوْ أَنْزَلْتَهُ في كِتَابِكَ أَوْ عَلَّمْتَهُ أَحداً مِن خَلْقِكَ أَوِ اسْتَأْثَرْتَ بِه في علم الْغَيْبِ عِنْدَكَ أَنْ تَجْعَلَ الْقُرْآنَ العظيمَ رَبيع قَلْبي ونورَ صَدْرِي وجلاءَ حُزْنِي وَذَهَابَ هَمِّي

“Ee Allaah! Hakika mimi ni mtumwa Wako, mtoto wa mtumwa Wako na mtoto wa mjakazi Wako. Utosi wangu uko Mikononi Mwako. Yaliyopita kwangu yako katika hukumu Yako. Hukumu Yako ni adilifu kwangu. Nakuomba kwa kila Jina ambalo ni Lako ulilojiita Kwako mwenyewe au uliloliteremsha katika Kitabu Chako au ulilomfundisha yeyote katika viumbe Vyako au ulilolikhusisha Wewe mwenyewe katika Elimu iliyojificha kwako, ujaalie Qur-aan tukufu iwe ni nguvu ya roho yangu na nuru ya kifua changu inayotoa huzuni wangu na kuondoka majonzi yangu”

isipokuwa Allaah Ataondosha majonzi na huzuni wake na kumbadilishia sehemu yake kwa faraja.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Dhuun-Nuun alipomezwa na nyangumi aliomba du´aa kwa kusema:

لَّا إِلَهَ إِلَّا أَنتَ سُبْحَانَكَ إِنِّي كُنتُ مِنَ الظَّالِمِينَ

“Hapana mungu wa haki asiyekuwa Wewe! Kutakasika na mapungufu ni Kwako! Hakika mimi nilikuwa miongoni mwa madhalimu.”[2]

Hakuna muislamu yeyote atakayeomba hivo isipokuwa Allaah atamwitikia.”

Baada ya Yuunus (´alayhis-Salaam) kusema du´aa hiyo Allaah (Ta´ala) akasema:

فَاسْتَجَبْنَا لَهُ وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْغَمِّ ۚ وَكَذَٰلِكَ نُنجِي الْمُؤْمِنِينَ

”Basi Tukamuitikia na tukamuokoa kutokamana na dhiki – na namna hiyo tunavyowaokoa waumini.”[3]

Hapana vibaya  mtu akajifanyia matabano mwenyewe, kwani hakika Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya hivo kabla ya kulala. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa akilala kila usiku alikuwa akikusanya vitanga vyake, akivitemea cheche za mate na akisoma ndani yake: “Qul huwaAllaahu ahad”, “Qul a´udhubi Rabbil-Falaq” na “Qul a´udhubi Rabbin-Naas”.” Kisha anajipangusa navyo mwili wake kadri na anavyoweza. Akianza kwa kichwa chake, uso wake na sehemu ya mbele ya mwili wake. Alikuwa akifanya hivyo mara tatu.”[4]

[1] Ahmad (1/391).

[2] 21:87

[3] 21:88

[4] al-Bukhaariy (5016) na Muslim (2192).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/465-466)
  • Imechapishwa: 27/07/2026