Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Tunachokusudia hapa ni kuzindua juu ya misingi mibovu ya ´Aqiydah ambayo imepelekea kupotoka kutokana na elimu na kuamini yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
MAELEZO
Kusudio la Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) kwa yale aliyoyataja katika fatwa hii ni kubainisha I´tiqaad ya watu wanaopindisha maana na wale wanaofata ujinga, kuonyesha kuwa ni I´tiqaad potofu na ya batili. Hili ndilo kusudio lake. I´tiqaad na misingi waliyojiwekea wenyewe na kuwaamrisha watu warejee kwayo ndiyo iliyoharibu akili, ikaharibu imani na kuzuia elimu, kwa sababu elimu ni kujua yale yaliyomo ndani ya Qur-aan na Sunnah. Ndiyo maana Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
Basi izingatie na uitafakari Qur-aan ikiwa unataka uongofu
kwa kuwa elimu ipo chini ya kuizingatia na kuitafakari Qur-aan[1]
Amesema pia (Rahimahu Allaah):
Elimu ni Allaah amesema, Mtume Wake amesema na Maswahabah wamesema –
hao ndio wenye maarifa[2]
[1] an-Nuuniyyah (1/315).
[2] an-Nuuniyyah (2/279).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 271
- Imechapishwa: 28/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Tunachokusudia hapa ni kuzindua juu ya misingi mibovu ya ´Aqiydah ambayo imepelekea kupotoka kutokana na elimu na kuamini yale aliyokuja nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
MAELEZO
Kusudio la Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) kwa yale aliyoyataja katika fatwa hii ni kubainisha I´tiqaad ya watu wanaopindisha maana na wale wanaofata ujinga, kuonyesha kuwa ni I´tiqaad potofu na ya batili. Hili ndilo kusudio lake. I´tiqaad na misingi waliyojiwekea wenyewe na kuwaamrisha watu warejee kwayo ndiyo iliyoharibu akili, ikaharibu imani na kuzuia elimu, kwa sababu elimu ni kujua yale yaliyomo ndani ya Qur-aan na Sunnah. Ndiyo maana Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) amesema:
Basi izingatie na uitafakari Qur-aan ikiwa unataka uongofu
kwa kuwa elimu ipo chini ya kuizingatia na kuitafakari Qur-aan[1]
Amesema pia (Rahimahu Allaah):
Elimu ni Allaah amesema, Mtume Wake amesema na Maswahabah wamesema –
hao ndio wenye maarifa[2]
[1] an-Nuuniyyah (1/315).
[2] an-Nuuniyyah (2/279).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 271
Imechapishwa: 28/07/2026
https://firqatunnajia.com/165-hapa-ndipo-utapata-elimu-na-uongofu/