Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwa sababu ambaye anamfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si mwenye kufahamu maana ya Qur-aan iliyoteremshwa kwake, wala Jibriyl si mwenye kujua sifa nyenginezo, basi hakuifanya kuwa kuwa ni mwongozo wala ubainifu wowote kwa watu.
MAELEZO
Hapa wanakusudiwa Mufawwidhwah, ambao wanadai kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui maana za Aayah. Makusudio ya wahy ni kinyume cha akili, nayo ni dalili za Qur-aan. Nao ni wayh. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema mwanzoni mwa Suurah ”al-Baqarah”:
ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ
”Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake ni mwongozo kwa wachaji.”[1]
Amesema katikati ya Suurah ”al-Baqarah”:
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ
“Mwezi wa Ramadhaan ambao [kumeanzwa] kuteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu… ”[2]
Hapa uongofu umetajwa kwa jumla. Katika Aayah ya kwanza uongofu unahusiana na kuafikishwa na kukubali. Katika Aayah ya pili uongofu unahusiana na mwongozo na ubainifu. Kwa hiyo ndani ya Qur-aan kuna aina mbili za uongofu:
1 – Uongofu wa maelekezo na uongozaji. Huu ni uongofu unaowahusu watu wote, muumini na kafiri.
2 – Uongofu wa kuwafikishwa na kukubali. Huu ni uongofu unaowahusu waumini pekee, kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):

”Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake ni mwongozo kwa wachaji.”
[1] 2:2
[2] 2:185
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 272
- Imechapishwa: 28/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kwa sababu ambaye anamfanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) si mwenye kufahamu maana ya Qur-aan iliyoteremshwa kwake, wala Jibriyl si mwenye kujua sifa nyenginezo, basi hakuifanya kuwa kuwa ni mwongozo wala ubainifu wowote kwa watu.
MAELEZO
Hapa wanakusudiwa Mufawwidhwah, ambao wanadai kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hajui maana za Aayah. Makusudio ya wahy ni kinyume cha akili, nayo ni dalili za Qur-aan. Nao ni wayh. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema mwanzoni mwa Suurah ”al-Baqarah”:
ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ
”Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake ni mwongozo kwa wachaji.”[1]
Amesema katikati ya Suurah ”al-Baqarah”:
شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ
“Mwezi wa Ramadhaan ambao [kumeanzwa] kuteremshwa humo Qur-aan ili iwe mwongozo kwa watu… ”[2]
Hapa uongofu umetajwa kwa jumla. Katika Aayah ya kwanza uongofu unahusiana na kuafikishwa na kukubali. Katika Aayah ya pili uongofu unahusiana na mwongozo na ubainifu. Kwa hiyo ndani ya Qur-aan kuna aina mbili za uongofu:
1 – Uongofu wa maelekezo na uongozaji. Huu ni uongofu unaowahusu watu wote, muumini na kafiri.
2 – Uongofu wa kuwafikishwa na kukubali. Huu ni uongofu unaowahusu waumini pekee, kama Alivyosema Allaah (Ta´ala):
ذَٰلِكَ الْكِتَابُ لَا رَيْبَ ۛ فِيهِ ۛ هُدًى لِّلْمُتَّقِينَ
”Hiki ni Kitabu kisicho na shaka ndani yake ni mwongozo kwa wachaji.”
[1] 2:2
[2] 2:185
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 272
Imechapishwa: 28/07/2026
https://firqatunnajia.com/166-uongofu-aina-mbili-ndani-ya-qur-aan/