Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Isitoshe watu hawa wanapinga kabisa akili kwa sampuli zake zote. Wanaona kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na ummah wake hawakuwa na maarifa juu ya Allaah (´Azza wa Jall) ya akili wala yaliyoteremshwa. Kwa maana nyingine katika hili wameshirikiana na wakanamungu kwa njia nyingi. Wote wamekosea pale wanapomnasibishia ujinga Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Salaf.

MAELEZO

Hata yale ya kiakili wanayodai kuwa ndani yake mna dalili, nayo pia wanayapinga. Qur-aan imekuja na dalili za kiakili:

قُلِ انظُرُوا مَاذَا فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

”Sema “Tazameni yaliyoko mbinguni na ardhini.”[1]

Hii ni dalili ya kiakili kwamba uutazame ulimwengu huu na viumbe vilivyomo ndani yake, kisha utoe dalili kwa hayo juu ya Muumba wake na kwamba Yeye pekee ndiye anayestahiki kuabudiwa. Hivyo Qur-aan ina dalili za kiakili. Qur-aan haikuifuta akili:

أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ

“Je, hawaizingatii Qur-aan?”[2]

Kutafakari ni kule kufikiri kwa akili.

Mufawwidhwah wameenda sambamba na mazanadiki ambao wanasema kuwa Qur-aan haiko juu ya dhahiri yake na kwamba inayo maana ya nje ya maana ya ndani. Mufawwidhwah wanasema kuwa dhahiri yake ni kuthibitisha sifa za Allaah, lakini ukweli wa mambo sivyo. Kwa hiyo Qur-aan haiko juu ya maana yake ya dhahiri kwa mujibu wao.

Amemaliza (Rahimahu Allaah) kwa kuweka misingi katika utangulizi huu mkubwa. Sasa atahamia katika kutaja mifano ya maneno ya Salaf kuhusu kuthibitisha majina na sifa za Allaah.

Allaah ndiye anayejua zaidi. Swalah na amani zimshukie Nabii wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah wake.

[1] 10:101

[2] 47:24

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 273
  • Imechapishwa: 28/07/2026