Hakika sifa njema zote ni za Allaah, tunamsifu, tunamwomba msaada tunamwomba msamaha. Tunajilinda kwa Allaah dhidi ya shari za nafsi zetu na dhidi ya ubaya wa matendo yetu. Ambaye Allaah amemuongoza, basi hakuna wa kumpoteza, na ambaye amempoteza, basi hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia kwamba hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee, hana mshirika. Nashuhudia ya kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, ambaye amemtuma kwa uongozi na dini ya haki ili ishinde dini zote, ijapokuwa watachukia makafiri.
Ama baada ya hayo;
Hakika kilichonifanya nichague mada hii ni mambo kadhaa ambapo miongoni mwa muhimu zaidi:
1 – Ummah wa Kiislamu umetofautiana katika nyanja mbalimbali za kiitikadi na nyenginezo. Mgawanyiko huu, pamoja na kukosa kurejea katika Qur-aan na Sunnah, umepelekea katika maafa ambayo uzito wake na athari zake mbaya anazijua Allaah pekee. Mpasuko huu ni mkubwa kutokana na kutengana kwao, moto wa mifarakano na mizozo baina yao kuwaka. Kisha maadui wa Uislamu kuwashinda na kuvamia nchi zao, kuwavunjia heshima yao, kuwatumikisha na kuwadhalilisha.
2 – Kuwepo kwa mikondo ya kimawazo iliyoibuka katika uga wa Kiislamu kwa njia na mitazamo mbalimbali ya kutaka kurekebisha hali ya ummah na kuuokoa.
Miongoni mwao wa kisiasa, wa kiakili na wa kiroho. Kila mmoja wa wafuasi wa mikondo hii anadai kuwa huo ndio msimamo sahihi wa Kiislamu unaopaswa kufuatwa na kwamba hakuna cha kuuokoa ummah isipokuwa huo. Sababu hizi mbili, pamoja na nyinginezo, zimenisukuma kutekeleza wajibu miongoni mwa wajibu mkubwa zaidi na muhimu zaidi. Nao ni kubainisha mwenendo wa Manabii katika kulingania kwa Allaah kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah na kubainisha sifa zake ambazo hakuna anayeshirikiana nazo na kubainisha ulazima wa kufuata mwenendo huo pekee, kwa sababu hii ndio njia ya kipekee inayomfikisha mtu kwa Allaah na kupata radhi Zake. Aidha ndio njia pekee ya kuuokoa ummah na inayowafikisha katika uongozi ulimwenguni na furaha Aakhirah.
- Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy ´Umayr al-Madkhaliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Manhaj-ul-Anbiyaa’ fiyd-Da´wah ilaa Allaah, uk. 27-28
- Imechapishwa: 28/07/2026

Muhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy ´Umayr al-Madkhaliy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Manhaj-ul-Anbiyaa’ fiyd-Da´wah ilaa Allaah, uk. 27-28
Imechapishwa: 28/07/2026
https://firqatunnajia.com/01-mfumo-pekee-wenye-kuokoa-ummah/