Swali: Una nasaha gani kuwapa wanaume kwa jumla na wanawake kuhusiana na swalah ya Fajr?
Jibu: Namnasihi kila muislamu kuichunga swalah ya Fajr na nyenginezo. Kwa sababu swalah ndio nguzo ya dini na ndio ´ibaadah muhimu zaidi baada ya shahaadah mbili. Yeyote mwenye kuiacha amekuwa kafiri na ambaye ataizembea basi yuko khatarini. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا
“Wakafuata baada yao waovu walipoteza swalah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu Motoni. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akafanya mema.”[1]
Endapo watatubia, wakaamini na wakatenda mema basi nataraji kuwa wataingia miongoni mwa wale Allaah kawaahidi:
فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا
“Basi hao wataingia Peponi na wala hawatodhulumiwa chochote.”[2]
[1] 19:59-60
[2] 19:60
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/124)
- Imechapishwa: 28/07/2026
Swali: Una nasaha gani kuwapa wanaume kwa jumla na wanawake kuhusiana na swalah ya Fajr?
Jibu: Namnasihi kila muislamu kuichunga swalah ya Fajr na nyenginezo. Kwa sababu swalah ndio nguzo ya dini na ndio ´ibaadah muhimu zaidi baada ya shahaadah mbili. Yeyote mwenye kuiacha amekuwa kafiri na ambaye ataizembea basi yuko khatarini. Allaah (Ta´ala) amesema:
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا إِلَّا مَن تَابَ وَآمَنَ وَعَمِلَ صَالِحًا
“Wakafuata baada yao waovu walipoteza swalah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu Motoni. Isipokuwa yule aliyetubu na akaamini na akafanya mema.”[1]
Endapo watatubia, wakaamini na wakatenda mema basi nataraji kuwa wataingia miongoni mwa wale Allaah kawaahidi:
فَأُولَـٰئِكَ يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ وَلَا يُظْلَمُونَ شَيْئًا
“Basi hao wataingia Peponi na wala hawatodhulumiwa chochote.”[2]
[1] 19:59-60
[2] 19:60
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/124)
Imechapishwa: 28/07/2026
https://firqatunnajia.com/nasaha-za-jumla-kuhusiana-na-fajr/