Amesahau kulipa swalah kwa kuzipangilia

Swali: Je, ule uwajibu wa kupangilia swalah unadondoka kwa sababu ya kusahau na ujinga?

Jibu: Wanazuoni wamekinzana juu ya suala hili. Maoni sahihi ni kwamba unadondoka kwa sababu ya ueneaji wa maneno Yake (Ta´ala) pale aliposema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Vilevile Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ummah wangu umesamehewa makosa, usahaulifu na yale wanayotenzwa juu yake.”[2]

[1] 2:286

[2] at-Twabaraaniy katika ”al-Awsatw” (8274), al-Bayhaqiy (11787) na Abu Nu´aym (6/352). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaamiy´” (7110).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/220-221)
  • Imechapishwa: 28/07/2026