391. Roho ya maiti fulani iko baina yetu?

Swali: Wakati baadhi ya watu wanapofanya matendo mema wanasema kuwa roho ya maiti fulani iko baina yetu?

Jibu: Maneno haya hayana haja kwa sababu mtu hunuia kumfanyia matendo mwingine kabla ya kuanza kuyafanya. Nia yake moyoni inatosheleza kutokamana na kutamkwa. Hata hivyo hapana vibaya endapo atasema: “Ee Allaah! Jaalia thawabu za matendo yangu yaende kwa fulani.”

Lakini maneno yao “roho ya maiti fulani iko baina yetu” hayajuzu. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَلاَ تَقْفُ مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ إِنَّ السَّمْعَ وَالْبَصَرَ وَالْفُؤَادَ كُلُّ أُولئِكَ كَانَ عَنْهُ مَسْؤُولاً

“Na wala usiyafuate yale usiyokuwa nayo elimu. Hakika masikio na macho na moyo, vyote hivyo vitaulizwa.” (17:36)

Hatujui kama kuwa roho ya fulani iko kati yetu au kwetu. Kwa ajili hiyo msemo huo unaingia katika yale Allaah aliyokataza.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/454)
  • Imechapishwa: 27/07/2026