Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Allaah (Ta´ala) anasema: “Nimewaandalia waja Wangu wema yale ambayo hajaonwa na jicho lolote, hayajasikiwa na sikio lolote na wala hayapita kwenye moyo wa yeyote.”[1]
Vivyo hivyo utambuzi wa wakati wa Saa na mfano wake. Ni miongoni mwa tafsiri ya mambo ambayo hakuna ayajuaye isipokuwa Allaah, ingawa tunafahamu maana ya yale tunayozungumzishwa na pia tunafahamu makusudio ya maneno hayo. Allaah (Ta´ala) amesema:
أَفَلَا يَتَدَبَّرُونَ الْقُرْآنَ أَمْ عَلَىٰ قُلُوبٍ أَقْفَالُهَا
“Je, hawaizingatii Qur-aan au nyoyoni mwao mna kufuli?”[2]
أَفَلَمْ يَدَّبَّرُوا الْقَوْلَ
”Je, hawakuzingatia kauli?”[3]
Kwa hivyo akaamrisha kuizingatia Qur-aan yote na si kuizingatia sehemu yake tu. Abu ´Abdir-Rahmaan as-Sulamiy amesema:
“Wale ambao walikuwa wakitusomesha Qur-aan – ´Uthmaan bin ´Affaan, ´Abdullaah bin Mas´uud na wengineo – wametueleza kwamba: “Baada ya kuhifadhi Aayah kumi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tulikuwa hatuzivuki mpaka tujifunze elimu yazo na kuzitendea kazi.” Tukajifunza Qur-aan, elimu na matendo.”[4]
Mujaahid amesema:
“Nimeisoma Qur-aan yote mara tatu mbele ya Ibn ´Abbaas; nikisimama katika kila Aayah na nikimuuliza kwayo.”
ash-Sha´biy amesema:
“Hakuna yeyote aliyezua uzushi isipokuwa ndani ya Qur-aan kuna ubainifu wake.”
Masruuq amesema:
“Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawakuulizwa juu ya chochote ndani ya Qur-aan isipokuwa elimu yake ilikuwa ndani ya Qur-aan. Hata hivyo elimu yetu haikuyafikia.”
Mlango huu ni mpana na umefafanuliwa zaidi maeneo mengine.
MAELEZO
Hakuna anayejua hakika kamili ya yale ambayo Allaah Amewaandalia waja Wake Peponi isipokuwa Allaah. Hata kama Amewaeleza majina yake na maana zake duniani, lakini hakika yake haijulikani isipokuwa na Allaah.
Yeye (Subhaanah) Ametuambia kwamba Saa itasimama. Saa ndiyo mwisho wa dunia na mwanzo wa Aakhirah. Lakini itasimama lini? Allaah ndiye anayejua. Hakuna Nabii aliyetumwa wala Malaika aliyekaribishwa anayejua wakati wake. Hakuna anayejua muda wa kusimama kwa Saa isipokuwa Allaah, kwa sababu hakuna maslahi kwetu kujua wakati wake. Maslahi ni kujua kwamba lazima itasimama ili tujiandae kwa ajili yake.
[1] al-Bukhaariy (4776) na Muslim (2824).
[2] 47:24
[3] 23:68
[4] Ahmad (5/410).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 269-270
- Imechapishwa: 27/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 269-270
Imechapishwa: 27/07/2026
https://firqatunnajia.com/164-namna-hii-ndio-salaf-walijifunza-qur-aan/