Swali: Je, kuthibiti kwa kuritadi kuna masharti yanayofaa kuzingatiwa?

Jibu: Masharti ya kuritadi:

Mosi: Mtu asiwe ni mwenye kupewa udhuru kwa sababu ya ujinga. Kwa mfano hakufikiwa na kitu, ameisha katika mazingira yaliyo mbali kabisa na waislamu na hakusikia kitu na wala hakufikiwa na kitu. Huyu hahukumiwi kitu mpaka kwanza afikishiwe na afafanuliwe kwamba jambo hili ni shirki na kwamba ni kufuru.

Pili: Asitenzwe nguvu. Akilazimishwa kutamka neno la kufuru pamoja na kwamba wakati huohuo imani na ´Aqiydah yake ndani ya moyo ni sahihi, huyu anapewa udhuru kwa ujinga:

إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُ مُطْمَئِنٌّ بِالْإِيمَانِ

”… isipokuwa yule aliyelazimishwa na huku moyo wake umetua juu ya  imani.” (an-Nahl 16:106)

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 57
  • Imechapishwa: 03/08/2018